Kongamano la tatu la maendeleo ya ushirikiano wa viwanda kati ya China na Afrika limefunguliwa leo hapa Beijing, na wajumbe zaidi ya 500 kutoka China na nchi za Afrika watafanya majadiliano kuhusu mustakabali wa maendeleo ya ushirikiano wa viwanda kati ya pande hizo mbili.
Katibu mkuu wa kongamano hilo Bw. Cheng Zhigang amesema, tangu lianzishwe, kongamano hilo limetoa ushauri kwa mashirika zaidi ya 500 ya China na Afrika, na kongamano la tatu litatoa mchango kwa ajili ya kutafuta fursa na njia mpya za ushirikiano kati ya China na Afrika.www.hakileo.blogspot.com
