Baada ya M23 sasa ni vikundi vingine vyenye silaha: UMKusikiliza



Herve Ladsous akiwa zairani Pinga Kivu Kaskazini

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani ndani ya Umoja wa Mataifa Herve Ladsous amesema baada ya utiwaji saini wa makubaliano ya amani ya Kampala kati ya serikali na kundi la waasi wa M23 yanayotarajiwa kuleta matumaini ya amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC ,sasa ni wakati wa kushughulikia vikundi vingine.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York Bwana Ladsous amesema kufikiwa kwa makubaliano hayo ni hatua kubwa huku akikiri kwamba M23 lilikuwa kundi lenye nguvu na kusisitiza kwamba Umoja wa Mataifa umejipanga kwa kila hali kuhakikisha wanavishughulikia vikundi vingine vyenye silaha.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company