BARAZA la Madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, limemgomea Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri kuendelea na kikao chao kama walivyopanga tofauti na maelekezo ambayo yalitolewa kwamba shughuli hizo zisimame wakati wa kipindi cha Bunge.
Kabla ya kuanza rasmi kwa kikao hicho, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Mwendahasara Maganga, alisema amepokea simu kutoka kwa Mwanri na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu kuwa vikao vya baraza visifanyike au vifanyike pale tu wabunge wanapokuwepo.
Alisema aliambiwa kuwa sababu ya kutofanyika kwa vikao hivyo ni kuwaruhusu wabunge ambao wapo bungeni waweze kushiriki, lakini pia na madiwani nao wanapaswa kufuatilia vikao vya Bunge badala ya kuendelea na baraza lao.
Hata hivyo, Meya wa Manispaa hiyo, Jerry Silaa akitolea ufafanuzi jambo hilo, alisema kwa mujibu wa kanuni sehemu ya 3.8.1, hakuna mkutano wa kawaida wa halmashauri utakaofanyika kama wajumbe wake hawatakuwa nusu ya wote.
Alisema kikao hicho kitaendelea kwa kuwa idadi ya wajumbe wamezidi: “Viongozi wafahamu baadhi ya maamuzi wanayofanya yanatia shaka uamuzi wao. Hivi sasa nikianza kuahirisha kikao kwa kuwa fulani hayupo, tutaahirisha mara ngapi?” alihoji.
Baada ya Silaa kutoa kauli hiyo, alitangaza kufunguliwa rasmi kwa kikao hicho, ambacho wajumbe waliokuwepo walipiga meza kuashiria kuwa wamekubaliana na maelezo hayo.
Alisisitiza kuwa baraza hilo limeitishwa kwa mujibu wa kanuni za kudumu sehemu ya 2 ibara ya 3, hivyo halmashauri hiyo itaendelea kufanya vikao kwa mujibu wa kanuni.