Juhudi za kidiplomasia kuwashawishi viongozi wa Sudani Kusini zimeshika kasi, rais wa Kenya na waziri mkuu wa Ethiopia wapo Juba


Wananchi wa Sudani Kusini wakiomba hifadhi katika kambi za wanajeshji wa Umolja wa Mataifa
Na Ali Bilali

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn wamewasili mapema leo asubuhi nchini Sudani Kusini kujadiliana na rais wa taifa hilo Salva Kiir anaye kabiliw ana wakati mgumu wakati huu. Hayo yanajiri wakati mapigano yakiendelea kushuhudiwa katika mji wenye utajiri wa mafuta.
Duru kutoka nchini Sudani kusini zimearifu kwamba viongozi hao wamekutana faraghani na kiongozi wa Sudani Kusini kujaribu kuutafutia suluhu mzozo wa kivita ambao Umoja wa Mataifa umesema watu zaidi ya mia sita wamepoteza maisha katika mapigano hayo yanayoendelea.

Jumuiya ya kimataifa, na mataifa jirani na Sudani Kusini yanazidisha juhudi za kidiplomasia ili kuumaliza mzozo huo ambao umeshadumu sasa zaidi ya juma moja unaowapambanisha wanajeshi wa serikali na waasi wanaomtii aliyekuwa makam wa rais Riek Mashar.

Tayari baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimia la kuongeza wanajeshi zaidi nchini humo wataofikia elfu kumi na mbili na mia tano.

Umoja wa Mataifa umetowa wito wa haraka juu ya kutowatolea msaada ma elfu ya wananchi waliokimbia makwao na ambao wamepewa hifadhi katika vituo mbalimbali vya majeshi ya Umoja wa Mataifa.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company