BAADHI ya viongozi wa dini hapa nchini wamebainisha kuwa kukithiri kwa migomo na matatizo mbalimbali ni dalili za watawala kushindwa kazi.
Wakihutubia kwenye mkesha na ibada ya Sikukuu ya Krismasi, viongozi hao walisema watawala wa sasa wamewasahau wananchi wao jambo ambalo ni hatari kwa taifa.
Walibainisha kuwa ung’ang’anizi wa madaraka bila kutimiza wajibu ni chanzo cha migogoro ndani ya tawala zao.
Akihutubia katika mkesha wa Sikukuu ya Krismasi, iliyoadhimishwa kitaifa katika Kanisa la Kalangala, mkoani Geita, Askofu Musa Magwesela wa Kanisa la African Inland Church (AIC) wa Jimbo la Geita, alisema watawala wamewasahau wananchi wao.
Alibainisha kuwa migomo ya walimu na madaktari inayotokea mara kwa mara inaonyesha watawala walivyo ving’ang’anizi wa madaraka bila kuwahudumia waliowapa madaraka hayo.
Askofu Magwesela, alisema viongozi wameshindwa kuishi maisha aliyoyaishi Yesu Kristo ambaye alikuwa akiwasaidia wananchi wao.
Alisema hofu ya Mungu haipo mioyoni mwao ndiyo maana wanatumia nguvu kujijengea uhalali wa kubakia madarakani.
Naye Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Damian Dallu ameonya kuwa rasilimali zilizopo nchini zisiwe sababu ya kuvunja muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwani Watanzania ni wamoja.
Amesema wanaoleta chokochoko za kuuvunja, na hata ikatokea ukavunjwa, bado Watanzania wataendelea kuitwa hivyo.
Akizungumza katika Ibada ya Misa Takatifu ya Sikukuu ya Krismasi iliyoadhimisha kwenye Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Amani, Askofu Dallu alisema viongozi wa dini wanakesha kuiombea amani Tanzania.
“Wengine waliposikia kuna mafuta katika upande mmoja wa Muungano walianza kusema ni yao… upande mwingine wa muungano hayawahusu, katika hili lazima tuombe,” alisema.
Aliongeza kuwa wanapotokea wanaopinga muungano watu wasiwachukie kwani wao wanaweza kuwa chanzo cha kuboresha changamoto zilizopo.
Akizungumzia kuhusu mchakato wa kuundwa Katiba Mpya, Askofu Dallu, alisema ni vema ukaendeshwa kwa haki, amani na upendo ili Tanzania waweze kuendelea kuishi kwa amani.
Kiongozi huyo aliwataka Watanzania kuacha uadui huku akiwasihi viongozi kukosa raha na kuwasaidia masikini pindi wanapowaona.
Alisema mali si silaha ya kumpa mtu amani bali inamwongezea wasiwasi na hofu.
Malasusa
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front, Alex Malasusa, amewataka viongozi kuacha tabia ya kung’ang’ania madaraka kiujanja ujanja kama ilivyokuwa enzi ya Nabii Herode.
Kauli hiyo aliitoa wakati alipokuwa akizungumza na waamini kwenye ibada ya kusherehekea kuzaliwa Yesu Kristo, iliyofanyika kwenye kanisa hilo jijini Dar es Salaam jana.
Alisema licha ya umri mkubwa walionao baadhi ya viongozi, wameendelea kung’ang’ania madaraka kama ilivyokuwa Nabii Herode, aliyetawaliwa na roho ya kishetani.
“Kutokana na ubinafsi, rushwa na tawala za kijanjajanja kama enzi za Herode, zimefanya dunia kutawaliwa na maovu kila kona pamoja na kulipizana visasi.
“Dunia hii leo imejaa maovu kila kona, watu wanatumia hela nyingi kwa ajili ya kujipatia silaha za kivita. Hali hiyo inatokana na watu kutotaka kuishi kwa amani,” alisema Askofu Malasusa.
Alisema kuna watu wako tayari kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kununua silaha za kulinda madaraka na kulipiza kisasi.
“Huu ni wakati wa jamii kuwaepuka baadhi ya watu ambao hawapendi kuwaona watu wakiishi kwa mshikamano na amani,” alisema.
Askofu Malasusa aliwataka watumie nyadhifa zao kutenda haki na kusimamia maendeleo ya kiuchumi katika jamii.
Nzigilwa
Askofu Msaidizi Mkuu wa Jimbo Kuu la Wakatoliki, Dar es Salaam, Dk. Eusebius Nzigilwa, alikerwa na viongozi wanaoshindwa kushindwa kupigania haki na badala yake wanajikusanyia mali.
Dk. Nzigilwa alisema viongozi wazuri ni wale walio tayari kupoteza nyadhifa zao kwa ajili ya kupigania haki ya walio wengi.
Aliwataka Watanzania kudumisha amani na mshikamano, hasa wakati wa hatua hii ya nchi kuelekea kwenye mchakato wa kupata katiba mpya.
Dk. Nzigilwa alisema anatarajia mambo yatakayoingizwa kwenye katiba hiyo yatakuwa ni yale yatakayoleta haki katika kusimamia rasilimali kwa ajili ya kukuza ustawi wa kila mmoja katika taifa.
Askofu Mhogolo
Askofu Godfrey Mhogolo wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Cetral Tanganyika, alisema watendaji wengi serikalini wameoza kimaadili.
Anasema amani inayoimbwa Tanzania haipo maana watu wanaishi maisha duni katikati ya watendaji waliojaa harufu ya rushwa.
Arusha
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Maombezi la Pentekoste, Mianziani, Hagai Varoya, aliwataka Watanzania kumgeukia Mungu na kuliombea taifa ili liepukane na mauaji yanayotokea mara kwa mara.
Alisema ukatili uliofanywa na vyombo vya dola dhidi ya raia wakati wa Operesheni Tokomeza Ujangili haupaswi kufumbiwa macho.
Alisema vyombo vya dola vyenye jukumu la kulinda wananchi vimeamua kuwatesa na wengine kuuawa, hivyo akawataka Watanzania kumgeukia Mungu ili amani na upendo vitawale.
Alibainisha kuwa kama kila mmoja akimgeukia Mungu mambo hayo yataisha kwani upendo utaongoza kwenye kila jambo hivyo muovu shetani hatapata mahali pa kujishika.
Muhoja Fabian
Paroko wa Parokia ya Bujora, Kisesa, Padri Muhoja Fabian, amehimiza viongozi na wananchi kuenzi amani na upendo ili waishi vizuri.