Mapigano ya kidini yanaendelea nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati huku Kundi la waasi la Séléka likitishia kuigawa nchi hio mara mbili


Wanajeshi wa Ufaransa na wale wa kikosi cha Umoja wa Afrika wa kiwapokonya silaha raia, mjini BanguiREUTERS/Alain Amontchi

Na RFI

Waasi wa Séléka wametishia kuigawa Jamuhuri ya Afrika ya Kati iwapo vita vya kidini havitokomeshwa.
“Kama hali itaendelea kua jinsi ilivyo, tutarudi kaskazini mwa nchi, sehemu tulikokoka, na nchi tutigawa mara mbili !” : Hayo ni maoni ya wafuasi wa kundi la zamani la waasi la Séléka, ambao wametishia kuigawa mara mbili Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Kwa upande wake, Abakar Sabone, aliekua mkuu wa waasi Séléka, ambae kwa wakati huu ni mshauri wa rais Michel Djotodia, amesema kua haoni wanachofanya kwa sasa, akibani kwamba ni vita visiokua na faida. Hayo ameyafahamisha jana katika mkutano na waandishi wa habari.

“Iwapo mazungumzo kati ya wakristo na waislamu yatafeli, itabi nchi tuigawe mara mbili : tutarejea kaskazini na wale watapendelea kusalia kusini watabaki, ili mradi tu amani ipatikane”, amesema Abakar Sabone.

Abakar Sabone, amebaini kwamba ameyasema hayo “kwa niaba ya jamii ya waislamu” na “wakuu wa Séléka”, ambao wako madarakani toka mwezi machi mwaka 2013, huku akizunguukwa na mawaziri wawili wa serikali.

Ametishia akisema kwamba iwapo suluhu haitopatikana katika kipindi cha wiki moja, waislamu wote watarudi kaskazini, ambako wengi wao walitokea.

“Tangazo hilo linamuhusu mwenyewe, halimuhusu rais Djotodia”, amesema leo asubuhi msemaji wa rais Michel Djotodia, Guy Simplice Kodégué, akibaini kwamba Jamuhuri ya Afrika ya Kati ni nchi moja, ambayo haiwezi ikagawanyika.

Abakar Sabone, anatoka kaskazini mashariki,ambae alikua pia mkuu wa kundi la waasi kabla ya kuteuliwa kama waziri katika utawala uliyon'golewa wa François Bozizé, ana wadhifa muhimu katika kundi la waasi la Séléka.

Tangazo alilotoa linaonyesha namana gani anawajibika katika kuunga mkono jamii ya waislamu wa Jamuhuri ya afrika ya Kati.

Kundi la waasi la Séléka lilionekana kaskazini mwa Jamuhuri ya afrika ya Kati mwishoni mwa mwaka 2012, baada ya kutengwa kwa muda mrefu katika nchi ambayo ina wakristo wengi.

Jeshi la Ufaransa lilitumwa hivi karibuni nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati katika operesheni iliyobatizwa “Sangaris”, ili kujaribu kuyapokonya silaha makundi yanayozimiliki.

Kundi la Séléka limeanza kupeleka wapiganaji wake katika mikoa ya Birao na Ndélé (kaskazini mashariki) ili kuongeza nguvu za kijeshi na silaha nzito nzito kwenye ngome zao.

Mapigano ya kidini ambayo yalikumba mji wa Bangui na kaskazini magharibi, yameanza kushuhudiwa wakati huu katika maeneo mengine.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company