Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowasa amewataka waendesha
bodaboda na watu wengine
wasimwite Rais kwa sababu
wanamtengenezea chuki na uhusiano
mbaya na watu.
“Mbona mnataka kuniletea uchuro!
Mnanitengenezea ugomvi na watu
jamani…,” alisema wakati akizindua
Shirikisho la Bodaboda Tanzania jana
kwenye Viwanja vya Leaders, Dar es
Salaam.
Lowassa amekuwa akitajwa kuwania
urais katika uchaguzi ujao wa Rais na
wabunge utakofanyika 2015. Hatua
hiyo imekuja baada ya Lowassa
kuwaeleza kuwa atafanya harambee
ya kuchangisha fedha ili kila aliyeingia
kwenye shirikisho la waendesha
bodaboda aweze kupata pikipiki yake.
Baada ya kauli hiyo waendesha
bodaboda hao walipaza sauti zao
wakiimba rais,rais …..wa mwaka
2015 huku wakidai amepita hana
mshindani. Aliwataka kuacha
kumwita rais kwa sababu
wanamtengenezea ugomvi na watu
Alisema asilimia 50 ya madereva
wanaoendesha bodaboda hizo siyo
pikipiki zao hivyo kutokana na hilo
atafanya harambee ili kila mmoja
kumiliki pikipiki yake ili waweze
kujiajiri wenyewe.
“Tumeona kuna tofauti kubwa kati ya
matajiri na maskini hivyo nimeona
kwenye shirikisho hili asilimia 50 siyo
za kwenu. Nimekusudia kuanzisha
harambee ya madereva ambao
hawana pikipiki ili nao wawe nazo
waweze kujiajiri,” alisema Lowasa.
Waendesha bodaboda
wakisukuma gari la Lowassa.
**
Lowasa aliitaka Kamati ya Shirikisho la
Bodaboda kukutana naye Januari 15
mwaka 2014 ili kupanga harambee
hiyo ifanyike lini na wapi.
Alisema matajiri nchini wapo wengi
nitawafuata na kuwachangisha
harambee wakiwemo Mwenyekiti wa
Kampuni za IPP, Reginald Mengi na
mfanyabiashara maarufu Said Salum
Bakhresa.