Rais Obama avionya vikosi vya uasi nchini Sudani Kusini


Rais wa Marekani Barack Obama .
REUTERS/Jonathan Ernst
Na Sabina Chrispine Nabigambo

Rais wa Marekani Barack Obama jana Jumamosi amevionya vikosi vya waasi nchini Sudan Kusini dhidi ya mapinduzi ya kijeshi baada ya wanajeshi wanne wa Marekani kujeruhiwa katika shambulizi dhidi ya ndege yao wakati wakijielekeza mjini Bor kwa shughuli za uokozi.
Taarifa ya ikulu ya Marekani imeeleza kuwa juhudi zozote za kunyakua madaraka kwa nguvu za kijeshi zitasababisha kukoma kwa msaada wa muda mrefu kutoka Marekani jumuiya ya kimataifa.

Rais Obama amesisitiza kuwa viongozi wa Sudani Kusini wanalo jukumu la kusaidia juhudi za Marekani kuwaokoa wamarekani na raia huko Juba na Bor mji ambao unashikiliwa na waasi.

Onyo la rais Obama linakuja baada ya ndege tatu za Marekani kushambuliwa kwa risasi wakati zikielekea huko Bor kusaidia juhudi za kuwaondoa wa Marekani nchini Sudani Kusini kufuatia kuchacha kwa mapigano baina ya serikali na waasi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company