WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII BALOZI KAGASHEKI AMEJIUZULU,PINDA ASEMA WENGI WA 4 KUFWATA


NA OSCAR SAMBA
Aliekuwa waziri wa utalii na mali asili Balozi Khamisi Juma Kagasheki leo usiku bungeni amejiuzu.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya kamati ndogo iliyoundwa na spika wa bunge Anne Makinda kuonesha ukatili uliofanyika kwenye operesheni iliyolenga kutokomeza ujangili hapa nchini.
Ripoti hiyo inaonesha jinsi jeshi la WJTZ lilivyo wa zalilisha wantazania kenye mikoa mbali mbali hapa nchini yenye ifadhi za taifa ikiwemo Morogoro,Karatu na maeneo ya mpanda.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ni kwamba watu walilazimishwa kujamiiana huku wengine wakishindikizwa kufanya mapenzi na miti pamoja na wanyama na mamia kuuwawa pia watanzania wengi wamebaki na ulemavu wa kudumu huku wengine wakiuguza majeraha hadi leo,Pia mifugo mingi iliuwawa  na mingine kutupwa mtoni.

Katika hatua nyingine waziri mkuu Peter Pinda mesema ya kwamba mawaziri wengine wa 4 wanaoshutumiwa kwenye ripoti hiyo wanatarajiwa kuchukuliwa hatua kama hizo pindi raisi atakapo wasili nchini.
Kwaundani wa taarifa hii endelea kutufwatilia
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company