Diwani wa CCM aingia matatani


Musoma. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, Ahamed Sawa, amechukua hati ya polisi inayoruhusu kukamatwa kwa Diwani wa Kata ya Kigera, kwa tuhuma za kuharibu vyumba vya madarasa.Inadaiwa kuwa kitendo hicho, kimesababisha wanafunzi zaidi ya 300 kushindwa kusoma.

Uamuzi huo umekuja baada ya mkurugenzi huyo kupata idhini ya madiwani wa halmashauri hiyo.
Mkurugenzi alidai kuwa diwani huyo Gabriel Ocharo kwa kushirikiana na kamati ya shule, aliezua jengo la vyumba madarasa sita kwa madai ya kutaka kufanya ukarabati wa vyumba viwili.

Alisema kitendo hicho hakikumsisha mtaalamu wa majengo wa halmashauri na kwamba huo ni ukiukwaji wa sheria.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company