Maziko ya Aliyekuwa Mbunge wa Chalinze Bwanamdogo kufanyika Bagamoyo leo



Mke wa aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, Said Bwanamdogo, Pili Mohamed (katikati) akiwa nyumbani kwake eneo la Makondeko Mbezi Dar es Salaam, jana. Picha na Michael Jamson.
Na Waandishi Wetu,Mwananchi
Bagamoyo/Pwani Mbunge wa Chalinze, Said Bwanamdogo anazikwa leo kijijini kwake, Miono Bagamoyo, maziko yanayotarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali.

Kifo cha mbunge huyo ni pigo la pili ndani ya mwezi mmoja baada ya kufariki kwa aliyekuwa Mbunge wa Kalenga, mkoani Iringa, Dk William Mgimwa.


Bwanamdogo alifariki dunia asubuhi ya juzi Hospitali ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (Moi). Ofisa Mwandamizi wa Bunge, Said Yakub alisema jana nyumbani kwa marehemu Miono Bagamoyo, kuwa mwili wa marehemu utaswaliwa asubuhi Msikiti wa Hospitali ya Muhimbili kabla ya kusafirishwa kwenda Bagamoyo.


Wanaotarajiwa kutoa salamu, ni Mwenyekiti wa Bunge, Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Serikali na wawakilishi wa vyama.


Hali ya mbunge huyo ilianza kubadilika tangu mwaka 2012, alisafirishwa kwa matibabu zaidi nchini India. Alitibiwa kwa zaidi ya miezi tisa, kabla ya kurejeshwa baada ya familia yake kuomba aendelee na matibabu nchini.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company