Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mbeya, Crispin Meela amewataka wananchi wa vijiji 35 vya wilaya hiyo ambavyo vipo kwenye mradi wa kupelekewa umeme mapema mwaka huu kuanza kujiandaa kwa kuweka miundombinu iliyo bora kwenye nyumba zao.Meela alitoa kauli hiyo juzi wakati akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Ibungila Kata ya Malindo kwenye mkutano wa hadhara wakati akiwa kwenye ziara yake ya kikazi.
Alisema Serikali kupitia Mradi wa Wakala wa Umeme Vijijini (Rea), vijiji 35 vimebahatika kuingia kwenye mradi huo ambao utekelezaji wake utaanza Julai mwaka huu.
Pia aliwataka wabuni miradi ya kiuchumi itakayoendana na uwepo wa nishati hiyo.
