Amchinja mke baada ya kunyimwa unyumba

Tabora. Mkazi wa mmoja wa Nzega, mkoani Tabora, Juma Kiyabo (45) amemchija mke wake, Wande Monera (34), kabla ya mwenyewe kunusurika kifo baada ya kujijeruhi vibaya shingoni katika jaribio la kutaka kujiua.
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Tazengwa saa 7 usiku wa Februari 16 mwaka huu, huku ikielezwa kuwa sababu ya tukio hilo ni kunyimana unyumba mara kwa mara.

Kaimu Kamanda wa Polisi, ambaye pia ni Mratibu Msaidizi mkoani Tabora, John Kauga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kaunga alisema taarifa za awali zinaonyesha kuwa, mtuhumiwa alikuwa akigombana na mkewe mara kwa mara kwa sababu ya kunyimwa unyumba kabla ya kuamua kuchukua hatua hiyo mbaya.

Kamanda Kaunga alisema kuwa, mtuhumiwa baada ya kufanya unyama huo, naye alijikata koo kwa lengo la kujiua, lakini hata hivyo jaribio lake lilishindikana na sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company