CHADEMA yaanza kufanyiwa hujuma Kalenga

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Grace Tendega, jana amechukua fomu ya kuwania kiti hicho huku msafara wake ukizuiliwa na polisi mkoani hapa kwa madai kuwa haukuwa na kibali cha kuandamana na kumshikilia Diwani wa Kata ya Mivinjeni, Frank Nyalusi.Msafara huo ulipokewa maeneo ya Igumbiro, kilometa nane kutoka Iringa mjini ukiwa unasindikizwa na pikipiki zaidi ya 50 na magari ya M4C zaidi ya manne na magari mengine madogo sita na kusababisha msafara huo kusimama zaidi ya saa moja baada ya polisi kuuzuia katika Mlima Ipogoro.

Maofisa wa polisi waliofika kuzuia masfara huo walisema wasingeweza kuuruhusu kupita katikati ya mji kwa madai kuwa maandamano hayo ni batili, hali iliyoibua malumbano kati ya uongozi wa polisi na CHADEMA mkoani hapa.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company