BREAKING NEWS; Ikulu ya Ukraine imehamwa


Mambo yanabadilika haraka mjini Kiev, mji mkuu wa Ukraine, baada ya maafikiano ya Ijumaa kumaliza msukosuko mkubwa wa nchi hiyo.
Bunge limepiga kura kumtoa gerezani kiongozi wa upinzani, Yulia Tymoshenko, baada ya washirika wake wawili kuteuliwa kuwa spika wa bunge na waziri wa mambo ya ndani ya nchi.Spika mpya, Alexander Turchinov, ndiye atayeratibu shughuli za serikali hadi utawala mpya utapoundwa.
Wanaharakati wa upinzani wamedhibiti milango ya ofisi za serikali katika mji mkuu pamoja na ikulu ya rais, kilomita 15 nje ya mji.

Wanaharakati piya wanataka uchaguzi ufanywe ufikapo mwezi May.
Huku nyuma, msaidizi wa Rais Yanukovych amesema rais sasa yuko mji wa Kharkiv, mashariki mwa nchi
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company