
Mambo yanabadilika haraka mjini Kiev, mji mkuu wa Ukraine, baada ya maafikiano ya Ijumaa kumaliza msukosuko mkubwa wa nchi hiyo.
Bunge la Ukraine limepiga kura kumshtaki Rais Yanukovych.Na wabunge piya wametaja siku ya uchaguzi mpya kuwa tarehe 25 May.
Baada ya hatua hizo kupitishwa wabunge walipiga makofi na kuimba wimbo wa taifa.
Na hapo awali bunge limepiga kura kumtoa gerezani kiongozi wa upinzani, Yulia Tymoshenko, baada ya washirika wake wawili kuteuliwa kuwa spika wa bunge na waziri wa mambo ya ndani ya nchi.
Spika mpya, Alexander Turchinov, ndiye atayeratibu shughuli za serikali hadi utawala mpya utapoundwa.
Huku nyuma, msaidizi wa Rais Yanukovych amesema rais sasa yuko mji wa Kharkiv, mashariki mwa nchi