Nchi changa zapata makadinali kadha


Makadinali 19 wepya wa Kanisa Katoliki wametawazwa leo katika sherehe iliyofanywa Vatikani - uteuzi wa kwanza kufanywa na Papa Francis tangu kuchukua uongozi wa Kanisa Katoliki.Ameteua viongozi wa kanisa kutoka nchi 12 zikiwemo Haiti, Burkina Faso na Ivory Coast ambao walivishwa majoho na kofia nyekundu.
Papa mstaafu, Benedict wa kumi na sita, naye alihudhuria, akionekana kwenye ibada ya hadhara kwa mara ya kwanza tangu kustaafu.

Mwandishi wa BBC Vatikani anasema uteuzi wa makadinali aliofanya Papa Francis unaonesha amebadilisha dira kutoka Ulaya na kuelekea maeneo ambako Kanisa Katoliki lina nguvu, yaani Amerika Kusini na Kati na Afrika.

Na kadinali mwengine mpya ni mkuu wa Kanisa Katoliki la Uingereza na Wales, Askofu Vincent Nichol.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company