.jpg)
Dodoma. Baadhi ya wabunge wa CCM ambao ni wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wamepinga msimamo wa chama hicho unaowataka kutetea muundo wa Serikali mbili katika mijadala ya Bunge hilo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, wamesema hawaoni mantiki ya msimamo huo, kwa kuwa Katiba inayotengenezwa ni ya wananchi.
Habari kutoka katika kikao cha ndani cha CCM kilichofanyika juzi kati ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya na wabunge wa CCM, baadhi ya wabunge waliweka wazi msimamo wao wa kutaka Serikali tatu.
“Wapo wengi hawakubaliani na msimamo wa CCM wa kutaka watetee Serikali mbili na wanashikilia msimamo wa Serikali tatu, ambao ndiyo msimamo wa wananchi wao,” alisema mmoja wa wabunge aliyekaririwa kutoka katika kikao hicho.
Habari zilizovuja kutoka katika kikao hicho, miongoni mwa walioeleza msomamo huo ni Alphaxard Kangi Lugola wa Mwibara, ni miongoni mwa waliokuwa na msimamo mkali kuhusu jambo hilo.
Lugola alipohojiwa jana, alishikilia msimamo wake wa kutaka Serikali tatu akisema anafanya hivyo ili kulinda masilahi ya wananchi anaowawakilisha.
“Mimi kama Kangi Lugola kama mjumbe ninayesimamia walionituma, nataka Serikali tatu… Hapa kuna mambo mawili, msimamo wa chama na msimamo wa mimi kama mwakilishi,” alisema.
Lugola aliongeza, “Msimamo huu nitautoa pia kwenye Bunge la Katiba na nitajenga hoja halafu Bunge kama chombo kitaweka mizania, ni muundo upi wa Serikali upite.”
Inadaiwa Christopher Ole Sendeka wa Simanjiro alikwenda mbali zaidi na kumweleza Rais Kikwete kwamba hakuna dhambi kubwa aliyotenda kama kuruhusu Zanzibar kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Kwa mujibu wa habari hizo, Sendeka alisema matatizo yote yanayoibuka sasa kuhusu muundo wa Serikali, yanatokana na marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ambayo yalivunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 ndiyo yaliyosababisha Zanzibar kutambuliwa kama nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuruhusu Rais wa Zanzibar kuwa na uwezo wa kuigawa mipaka ya Zanzibar, jukumu ambalo ni la Rais wa Muungano.
Alipoulizwa kuhusu madai hayo jana, Sendeka, alikataa kueleza lolote akisema kikao hicho kilikuwa ni cha faragha.
Mbunge mmoja kutoka Kanda ya Ziwa ambaye hata hivyo hakutaka jina lake litajwe, aliliambia gazeti hili kuwa kwa uchache, theluthi mbili ya wabunge wa CCM wanataka Serikali tatu.
“Subirini muone moto utakaowaka bungeni siku tutakapofika kwenye hicho kipengele cha Muungano, nadhani halitatosha, tumeamua kusimama na wananchi siyo msimamo wa CCM,” alidokeza.
Mjumbe huyo alisema yeye ataeleza wazi kuwa haungi mkono muundo wa Serikali ya CCM unaotaka Serikali mbili na kwamba yuko tayari kukabiliana na adhabu yoyote kama CCM itaona amefanya makosa.
Mbunge wa Beatrice Shelukindo wa Kilindi ambaye pia ni mjumbe wa Bunge hilo, alisema awali alikuwa muumini wa Serikali tatu lakini baada ya kuelimishwa, amebadili msimamo huo.
“Ni kweli wapo wana CCM wanataka Serikali tatu, hata mimi nilikuwa huko lakini baada ya kuelimishwa nakubali muundo wa Serikali mbili pale tu kero za Muungano zitakapotatuliwa,” alisema.
Alitoa mfano wa mbunge kutoka Zanzibar kuwekwa katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) wakati mambo yanayofanywa na kamati hiyo kwa asilimia 100 yanahusu upande wa Bara pekee.
Mbunge mwingine kutoka Kanda ya Ziwa ambaye naye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema ni usaliti kwa CCM kuwachagulia Watanzania aina ya Muungano baada ya kutoa maoni yao kuhusu jambo hilo.
“Mimi binafsi nataka Serikali mbili lakini siungi mkono kitendo cha chama changu kuweka msimamo wa pamoja na kutaka uwe ndiyo msimamo wa taifa kwani Katiba ni mali ya wananchi,” alisema na kuongeza:
Mgawanyiko huo wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, umekuja siku moja baada ya CCM kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kutangaza msimamo wa CCM kama taasisi kuwa ni muundo wa Serikali mbili na imewataka wajumbe wake kusimamia msimamo huo wakati wa mijadala bungeni.
Hata hivyo, Zainab Kawawa alitaka wajumbe wa Bunge la Katiba watakaokwenda kinyume na msimamo wa chama, wanyang’anywe kadi.