JK afikishwa The Hague, Adaiwa kutoa kauli za uchochezi

KITUO cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB) kimemshitaki Rais Jakaya Kikwete kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya binadamu (ICC), mjini The Hague, Uholanzi kwa madai ya kutoa kauli zenye kuhamasisha uvunjifu wa amani nchini.Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za kituo hicho zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TCIB, Deus Kibamba, alisema kauli ya Rais Kikwete kuwataka wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waamke na kujibu mapigo wanaposhambuliwa, ni uchochezi.

Alisema tayari ametoa taarifa kwa Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensuda, kumwomba atume timu yake nchini ili ifanye uchunguzi wa awali juu ya matamshi ya viongozi wakuu nchini.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company