
Kimaro, kukatwa mapanga, huku Mbunge wa Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbayi, akipandishwa kizimbani.
Wengine waliopandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuwajeruhi wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni pamoja na Diwani wa Kata ya Buselesele, wilayani Chato, mkoani Geita, Christian Kagoma na makada wengine 15 wanaodaiwa kuwa wa CHADEMA.
Washitakiwa hao walikamatwa juzi na kufikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Gadiel Mariki jana na kila mmoja kusomewa mashitaka sita.
Mwendesha Mashtaka wa Mahakama, Shukrani Madulu, alidai kuwa washtakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo juzi katika Kata ya Ubagwe.
Alidai kuwa washtakiwa hao wakiongozwa na Mbunge Kasulumbayi waliwashambulia kwa mapanga wafuasi wa CCM wakati wa kampeni za udiwani wa Kata ya Ubagwe iliyopo Halmashauri ya Ushetu.
Alidai kuwa katika vurugu hizo washtakiwa, pia walilishambulia gari la CCM la wilaya na kuliharibu.
Washtakiwa wote walikana mashtaka, lakini wamenyimwa dhamana kwa madai kuwa watu waliowajeruhi wako katika hali mbaya, kwani baadhi yao wamehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kahama. Kesi hiyo imeahirishwa hadi leo.
Kabla ya kufikishwa mahakamani, walioshuhudia vurugu hizo walieleza kuwa majeruhi hao walikumbwa na mkasa huo wakati wakiwa kwenye gari la CCM wilaya
ambalo pia lilikuwa na watuhumiwa watatu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa CHADEMA, waliokuwa wakipelekwa kituo kidogo cha Polisi Bulungwa.
Watuhumiwa hao walidaiwa kufanya fujo kwenye
mkutano wa kampeni wa Chama cha TADEA ambacho pia kimeweka mgombea wa udiwani katika Kata ya Ubagwe.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kahama watu 16 akiwemo Mbunge wa Maswa
Mashariki, Kasulunabayi, walikamatwa na Polisi wakidaiwa kuhusika na vurugu hizo.
Baadhi ya majeruhi waliolazwa kwenye Hospitali ya Halmashauri ya Mji
wa Kahama akiwemo dereva wa gari la CCM Wilaya ya Kahama, Charles Peter, walisema walipofika kwenye kizuizi hicho walisimama ndipo wafuasi wa
CHADEMA waliposhuka kwenye gari la mbunge huyo na kuanza kuwapiga.
Ilielezwa kuwa Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Alphonce Kimaro, alikumbwa na sekeseke hilo kwani alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa ndani ya gari la CCM akiwasindikiza watuhumiwa hao Polisi.
“Mtendaji huyo ni mmoja wa majeruhi waliojeruhiwa vibaya kwa kukatwa mapanga ovyo mwilini na watu wengine watano wamejeruhiwa katika tukio hilo na hali zao ni mbaya,” alisema Peter.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Halmashauri ya mji wa Kahama, Richard Mabagala, aliwataja majeruhi wengine kuwa ni pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM, Masuod Melimeli (34), Sebastian Masunga (34) na Ramadhani Salumu (24).
Wengine ni Subira Nyangusu, pamoja na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ubagwe, Kimaro na dereva wa gari la CCM, Peter.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Andrew
Emmanuel, Masunga Kamaro na Peter walisafirishwa kwenda Hospitali ya Bugando
jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.