NA MWANANCHI MTANDAONI
Dar es Salaam. Vigogo saba wa Suma-JKT wanaokabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wamepatikana kuwa na kesi ya kujibu na kutakiwa kuanza kutoa ushahidi wao wa utetea Machi 11 na 14 mwaka huu.
Akitoa uamuzi huo jana Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 10 wa upande wa mashtaka pamoja na vielelezo walivyoviwasilisha mahakamani hapo,amewaona washtakiwa hao wana kesi ya kujibu na kwamba wanapaswa kutoa ushahidi wao wa utetezi dhidi ya mashtaka yanayowakabili.
Washtakiwa hao ni Kanali,Ayoub Mwakang’ata, Luteni Kanali Mkohi Kichogo,Luteni Kanali Paul Mayavi,Meja Peter Lushika,Sajenti John Lazier, Meja Yohana Nyuchi na Mkurugenzi wa miradi ya matrekta wa Suma-JKT,Luteni Kanali Felex Samillan.
Uamuzi huo umetolewa baada ya Mwendesha Mashtaka wa Takukuru,Lizy Kiwia,Januari 15,2014 kufunga ushahidi uliotolewa na mashahidi wao 10.
Vigogo hao kwa pamoja wanadaiwa Machi 5, 2009 katika ukumbi wa Suma-JKT wakiwa wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Suma- JKT kwa makusudi walitumia madaraka yao vibaya
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago