Ratiba na utaratibu wa Bunge Maalum la Katiba haujatuwezesha kurejea kupata maoni ya mliotutuma au walau kuwekwa utaratibu wa Mwenyekiti wa Muda kuitisha mkutano wa kusikiliza umma/wadau (public/stakeholders hearing) hapa Dodoma.
Nilitoa pendekezo hili kwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge na kwa wadau; rejea:http://mnyika.blogspot.com/2014/02/kwanini-ni-muhimu-tushirikishe-wananchi.html nahttp://www.ippmedia.com/frontend/?l=64919
Hata hivyo, mjadala wa bungeni unaanza kesho na hatimaye kanuni kupitishwa kwa kile ambacho vyanzo vyangu vimenidokeza kuwa msimamo wa wenye madaraka ni kwamba “mamlaka ya kujitungia kanuni ni ya bunge maalum lenyewe, kutunga kanuni ni suala la ndani la wajumbe wenyewe”.
Kutokana na ukuu na upekee wa kanuni hizi katika uendeshaji wa Bunge Maalum, ni wazi kasoro katika kanuni zitaacha mianya ya maoni ya wananchi yaliyomo kwenye rasimu ya katiba kuchakachuliwa badala ya kuboreshwa.
Aidha, yapo mambo katika rasimu ya kanuni yanayohusu haki, kinga na maslahi ya wajumbe wa Bunge Maalum ambayo katika mizania ya utawala bora ni vyema katika kuyatunga maoni na mapendekezo ya wadau wengine wa nje ya Bunge la Maalum yakatolewa.
Tarehe 20 Februari 2014 vyombo vya habari vilimnukuu Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Pandu Kificho kwamba ameunda kamati ya muda ya kanuni ya kumshauri na kuahirisha vikao kutoa nafasi kwa kamati hiyo kufanya kazi na pia wajumbe kujisomea nakala ya rasimu za kanuni walizopewa.
Aidha, alitangaza kwamba mjadala wa rasimu ya kanuni hizo utaanza leo jumapili 23 Februari, 2014 na jumatatu tarehe 24 Februari 2014 na hatimaye kanuni kupitishwa. Katika mazingira hayo, njia ya haraka ya kuweza kuwasiliana na kupata maoni na mapendekezo ya wananchi na wadau ni kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) mathalani kupitia mitandao ya internet na simu za mkononi.
Hivyo, chukua hapa au popote kwingine nakala ya rasimu ya kanuni za Bunge maalum; soma, jadili na wenzako na fikisha maoni na mapendekezo kupitia TEHAMA kwa mjumbe anayekuwakilisha katika Bunge Maalum la katiba.
Kwa upande wa wananchi wa Jimbo la Ubungo na wengine mtakaopenda kushiriki pamoja nasi; nawakaribisha kwenye mkutano wa mtandaoni siku ya leo jumapili tarehe 23 Februari 2014.
Mkutano huo wa mbunge na wananchi utaanza saa 6 kamili mchana mpaka saa 8 mchana kupitia mtandao wa http:mnyika.blogspot.com. Mkutano utaendelea saa 2 usiku mpaka saa 4 usiku kwa mliokuwa wakazi wa Ubungo mlio nje ya nchi na pia kwa watakaokosa nafasi ya kushiriki mkutano wa mchana.
Jinsi ya kushiriki mkutano huo, pitia nakala ya rasimu iliyotolewa na uliza maswali au toa maoni na mapendekezo mara baada ya ujumbe huu. Nitapitia maoni na mapendekezo yenu nami nitachangia maoni na mapendekezo yangu wakati mkutano ukiendelea kupitia ukurasa huu.
Natanguliza shukrani nikitarajia kupata maoni na mapendekezo yenu ya kuboresha rasimu ya kanuni tuweze kupata nyenzo sahihi ya kuboresha au kufanya mabadiliko katika rasimu ya katiba tupate katiba bora.
Wenu katika uwakilishi wa wananchi,
John Mnyika (Mb)
23 Februari 2014
Bungeni, Dodoma