Benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya kuendelea kuipa mkopo serikali ya Uganda licha ya kusaini sheria ya kipiga marufu ndoa za watu wa jinsi moja


Makam mwenyekiti wa benki ya uwekezaji barani Ulaya Pim Vam Ballekom
Na Ali Bilali
Benki ya uwekezaji ya Umoja wa Ulaya, inasema kuwa itaendelea kuisaidia Uganda kwa kuwapa mikopo na kuwekeza katika sekta mbalimbali ili kuinua uchumi wao licha ya rais Yoweri Museveni kutia saini sheria inayopiga marufuku ndoa za jinsi moja nchini humo.
Marekani na Uingereza na Mataifa mengine ya Magharibi yametishia kusitisha misaada nchini Uganda, na tayari Benki ya Dunia imesitisha kutoa mkopo kwa serikali ya Kampala.
Makamu wa rais wa Benki hiyo ya uwekezaji Pim Van Ballekom ameongeza kuwa licha ya wao kuwa taasisi ya uwekezaji pia wanashauriana na tasisi mbalimbali za Umoja wa Ulaya kuhusu Uganda.

Akizungumza wakati akitowa mkopo wa Euro milioni 45 kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha sekta ya kilimo, makam mwenyekiti huyo amesema angependa miradi hiyo pia iendelee nchini Uganda wakati huu mazungumzo yakiendelea.

Uganda imejikuta matatani baada ya rais wa nchi hiyo kutia saini kwenye sheria inayopiga marufuku ndoa za watu wa jinsia moja, hatuwa iliopongezwa na wananchi wa taifa hilo, huku wanaharakati wakiipinga na kusema ni kinyume na haki za binadamu.

Awali serikali ya Uganda ilisema itaendelea kushikiana na kunzungumza na taasisi mbalimbali za kifedha juu ya hatuwa ya kuibana kiuchumi kutokana na kusainiwa kwa sheria hiyo.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company