Pandu Kificho akalia kuti kavu, Aandaliwa mashtaka, kutimuliwa Siri za kumchukia zaanza kuvuja

SIKU chache baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kubaini kuwa kina wakati mgumu katika mijadala na upitishaji wa vifungu vya rasimu ya katiba, kimeanza kutafuta mchawi.

Tayari chama hicho kimeshamshika uchawi Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, kwa kuwasilisha waraka wa maoni ya baraza hilo kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba yanayotaka serikali tatu, tofauti na msimamo wa chama chake kinachoamini katika serikali mbili.Waraka huo unapendekeza muundo wa Muungano unaotaka serikali za Tanganyika na Zanzibar ziwe na mamlaka kamili.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa Kificho aliundaa waraka huo bila kuwashirikisha viongozi wenzake wa baraza hilo na kuufikisha katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mei, 2 mwaka jana.

Katibu wa Kamati ya Wawakilishi wa CCM, Salmin Awadh Salmin, jana aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa kuwa Kificho ameuandaa waraka huo kwa siri, huku ukiwa na mambo yanayokinzana na msimamo wa chama chao cha CCM.

Salmin alisema msimamo wa CCM ni muundo wa serikali mbili, lakini Kificho aliwasilisha maoni ya Baraza la Wawakilishi yakionyesha wanahitaji serikali tatu.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company