
Zitto ameweka wazi msimamo wake jana kwenye kurasa zake za mitandao ya Facebook na Twitter akiwashauri wajumbe wa Bunge hilo kutoendelea na malumbano ya namna ya kupiga kura kati ya zile za siri au za wazi na badala yake kura ya wazi ipewe nafasi.
Alisema: “Nasikia kampeni zinaendelea Dodoma kuhusu uamuzi huo. Siasa zetu tunazifanya ni ‘zero-sum game’, kwamba anayepata anapata vyote, na anayekosa anakosa vyote, haipaswi kuwa hivyo hata kidogo.”