UJENZI WA BARABARA YA KIMARA HADI KIVUKONI WAENDELEA, KUKAMILIKA NDANI YA MIEZI SITA


Sehemu ya Magomeni jijini Dar es salaam ikonesha maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo

Kituo cha Magomeni Kagera
Daraja la Manzese pamebadilika

Daraja la waendao kwa miguu stendi ya mabasi ya bara ya Ubungo

Flyover ya waendao kwa miguu Ubungo

Kampuni ya Strabag International GmbH inayotekeleza ujenzi wa barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kivukoni jijini Dar es Salaam imetakiwa kuhakikisha kuwa inakamilisha ujenzi wa sehemu hiyo ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo kama mkataba wao unavyoelekeza.

Waziri wa Ujenzi Mhe. Magufuli alitoa agizo hilo wakati akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Dar es Salaam Bus Rapid Transit - BRT) ambao umeelezewa kuwa na changamoto nyingi kiasi cha kusababisha usumbufu kwa watumia barabara hiyo kwa kipindi kirefu.

Akimpatia taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale alimjulisha Waziri Magufuli kuwa kwa hivi sasa changamoto nyingi zimefanyiwakazi na mradi unaendelea kusimamiwa kwa karibu ili kuhakikisha kuwa hukuna ucheleweshaji zaidi katika hatua hii iliyobaki.

Mkataba wa ujenzi wa barabara hizi pamoja na vituo vya mabasi ulisainiwa mwezi Desemba mwaka 2012 ukiwa umepangwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu kwa gharama ya Shilingi bilioni 280.
CHANZO:MTAA KWA MTAA (MM)
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company