MFAHAMU Edward Sokoine,


Edward Moringe Sokoine
Edward Moringe Sokoine (1938 - 12 Aprili 1984) alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Tanzania.

Aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili, tangu tarehe 13 Februari 1977 hadi 7 Novemba 1980, tena tangu tarehe 24 Februari 1983 hadi kifo chake, alipofariki kufuatana na ajali ya gari.

Uongozi wake ulionekana kuwa wa mfano kwa jinsi alivyokuwa na uadilifu na kufuatilia utendaji kazi huku akikemea ulaji rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.

Sokoine alifariki kwa ajali ya gari wakati akitoka kwenye kikao cha bunge Dodoma kuelekea Dar es Salaam. Wengi wanashuku ajali hiyo kuwa ilipangwa.

Kifo chake kilileta majonzi makubwa kwa Watanzania wa kawaida ambao walikuwa wanamtarajia kuwatetea wanyonge na kuinua hali ya maisha yao.

Mwili wa Edward Moringe Sokoine ulizikwa nyumbani kwao Monduli, mkoani Arusha.

Chuo cha Kilimo na Mifugo Morogoro kilipewa jina la "Chuo cha Kilimo cha Sokoine" ambacho kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Sokoine.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company