Nigeria yasema Mugabe amewatusi


Mwanabalozi wa Zimbabwe nchini Nigeria ameitwa akajieleze kwa sababu ya matamshi ya Rais Robert Mugabe kuhusu rushwa.

Mwezi uliopita Rais Mugabe alilalamika kuwa Wa-Zimbabwe wanaanza kuwa kama Wa-Nigeria - wakitaka jambo lifanyike inabidi watie mkono mfukoni.

Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Nigeria imemwambia balozi wa Zimbabwe, Stanley Kunjeku, kwamba hawakubali shambulio hilo la kuwatusi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company