Nayasema haya kwani leo athuuri wamekatisha maelezo ya ufafanuzi ya watu wachache katika bunge la Muungano wa Tanznia kwa sababu Tindu Lissu alikuwa akiueleza ukweli umma kuhusu udhaifu wa serikali na Muundo wa Muungano ulivyo feki na kuwataka wanaccm kutokuendelea kuudanganya umma.
kwa kuwa runinga hii ni ya CCM na siyo ya Taifa waliamua kukatiza matangazo yao kama ilivyo desturi yao kwani muda huo huo nilimtarifu mwenzangu kwa kumwambia "TBC lazima wakate".
Ninalazimika kuamini ya kwamba sio tatizo la kiufundi kwani sio mara ya kwanza kwa runinga hii iliyopoteza mwelekeo kufanya upuuzi huu.
Mwaka 2010 katika kuhitimisha kampeni za chama cha CHADEMA uliofanyika pale jangwani walikata mara baada ya madongo kwa CCM pia mwaka jana wakati mbunge wa upinzani Mkosa Mali akichangia walimfanyia hivyo hivyo.
Sera ya TBC1 ni sera ya CCM kwani wao nao wanaunga mkono muundo wa serikali 2 ndio maana hata katika vipindi vyao huwalika wageni wanaounga mkono muundo wa erikali 2.
Kama hiyo haitoshi huenda kinyume na maadili ya uandishi wa habari yasiyo wataka kuegemea upande wote wote ule kwani watangazaji wao nao hugeuka na kuwa wachangiaji na pale anapoonge kitu cha kuponda sera za pande pinzani hucheka na hutikisa kichwaa.
Ipo siku niliwahi kushauri ya kwamba kituo hiki cha runinga ya faa sasa ibadilishe nembo yake na kutumia ile ya chama cha mapinduzi yaani CCM.
tbc yawapasa muelewe ya kwamba mpo kwa ajili ya watanzania na watanzania wapo wanaopenda miundo mbalimbali ya serikali.
Kwa hili nawataka watanzania wote kuisusia tv hii na kushindikiza mabadiliko amasivyo naiombe laana kali kutoka kwa MWENYEZI MUNGU kwa kumtaka ailani kuliko SHETANI.
(TIDO MUHANDO tuta kukumbuka daima)