TFF YAZITHIBITISHA NDANDA, STAND UNITED NA POLISI MORO KUPANDA LIGI KUU, PAMBA YAPOROMOKA HADI LIGI YA MKOA

Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limezithibitisha timu za Ndanda SC ya Mtwara, Polisi ya Morogoro na Stand United ya Shinyanga kupanda daraja kutoka la Kwanza, kwenda Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao.
Taarifa ya TFF kwa BIN ZUBEIRY leo, imesema timu tatu za Ligi Daraja la Kwanza zitacheza Ligi ya Mkoa katika mikoa yao msimu ujao baada ya kushika nafasi za mwisho katika makundi yao, hivyo kushuka daraja.

Prisons inaweza kuwa moja ya timu zitakazoshuka Daraja kuzipisha Ndanda, Polisi na Stand United

Transit Camp imeshika nafasi ya mwisho katika A wakati Mkamba Rangers imeshuka daraja kwa kukamata mkia katika kundi B. Nayo Pamba SC imerudi kucheza Ligi ya Mkoa wa Mwanza baada ya kuwa ya mwisho kwenye kundi C.
Timu zilizopanda daraja kutoka FDL kwenda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao ni Ndanda SC ya Mtwara kutoka kundi A, Polisi Morogoro ya kundi B na Stand United ya Shinyanga iliyoibuka kinara katika kundi C.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company