Ushindi wa CCM Chalinze waibua hisia mseto


Ushindi wa chama tawala CCM kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Chalinze umeibua mseto wa hisia miongoni mwa kada mbalimbali. Wasomi wanasema kuchaguliwa Ridhwan Kikwete kuwa mbunge mpya wa Chalinze ni ishara ya kuendelea kupanuka satwa na ushawishi wa chama hicho kikongwe nchini Tanzania. Wachambuzi wa kisiasa wanasema uchaguzi huo pamoja na chaguzi zingine ndogo zilizotangulia zinatumiwa na vyama vya siasa kujipima nguvu kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Profesa Benson Bana wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ameiambia Idhaa hii kwamba, vyama vya upinzani vimeshindwa kwenye uchaguzi huo kutokana na kufeli kuainisha barabara sera zao. Msomi huyo ameongeza kuwa, vyama vikubwa vya upinzani kama vile CHADEMA na CUF vinakabiliwa na migogoro ya ndani; jambo lililosababisha kushindwa kwao.

Ridhwan Kikwete ameshinda kwenye uchaguzi huo kwa kujipatia zaidi ya kura 20,000 huku mpinzani wake wa karibu, Mathayo Torongei wa CHADEMA akijipatia takriban kura 2500.

Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company