
Bi. Marzieh Afkham amesema Nigeria ni nchi muhimu magharibi mwa Afrika na ni jambo la kusikitisha kuona kuwa kwa muda sasa imekuwa ikisumbuliwa na makundi ya kigaidi ambayo yamevuruga usalama na utulivu wa Wanigeria mbali na kuisababishia nchi hiyo hasara. Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Iran ameelezea wasi wasi wake kuhusu makundi ya kigaidi kuwateka nyara wasichana Nigeria. Ameongeza kuwa kitendo kama hicho hakikubaliki kabisa na ameeleza kuwa ana matumaini hatua imara zitachukuliwa ili kuzuia uhalifu wa makundi yenye misimamo mikali na ya kigaidi huko Nigeria na ulimwengu mzima kwa jumla. Aidha ameelezea matumaini yake kuwa utulivu utarejeshwa haraka Nigeria.
Kuhusu mazungumzo ya nyuklia, Bi. Afkham amesema, mstari mwekundu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kutokiukwa haki isiyopingika na ya wazi ya watu wa Iran kuhusu umuliki wa teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani.