Na Oscar Samba
Kweli sasa ninaamini ya kwamba Taifa hili ni la watu wasiojali kwani kupanda kwa bei ya mafuta maranyingi kumekuwa kukipandisha na gharama za nauli kwa abiria lakini hivi sasa bei ya mafuta katika soko la dunia imeshuka.
kipindi cha robo ya mwisho wa mwaka kuanzia Septemba hadi Desemba mwaka jana, bei za mafuta ghafi zimekuwa zikishuka kwa kasi ikilinganishwa na kipindi cha nyuma, bei zimeshuka kutoka dola 100 (Sh 170,000) kwa pipa hadi kufikia wastani wa dola 60 (Sh 102,000) kwa pipa moja ambayo ni sawa na kushuka kwa bei kwa asilimia 40.
HAPA KWETU,mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa, imeshuka kuanzia leo, huku watumiaji wa petroli wakipata nafuu zaidi kutokana na kuuzwa chini ya Sh 2,000 baada ya kipindi cha muda mrefu.
Kutokana na kushuka kwa bei ambako pia kunachangiwa na kushuka kwa bei , sasa petroli itauzwa lita moja kwa Sh 1,955, dizeli itakuwa Sh 1,846 kwa kila lita moja na mafuta ya taa yatakuwa yanauzwa kwa Sh 1,833 kwa kila lita moja.(MM)
Cha ajabu uafadhali huu bado hauna tija kwa abiria wa vyombo hivyo kwani mamlaka husika kama Eura wamefanya kazi yao kazi imebaki kwa SUMATRA ambao kwa muda mwingi wamekuwa wakitazama tuu masilai ya wenye vyombo hivyo kuliko watanzania wanyonge wenye kutumia usafiri wa UMMA.
Labla niwakumbushe kwa kuwarudisha katika mfumo wa nchi yetu ambao upo tuu kikatiba na kusemwa midomoni huku ukipewa kisogo kiutendaji ya kwamba sisi ni taifa lenye kufwata siasa za kiuchumi za KIJAMAA mbazo asili yake na chimbuko lake ni unafuu kwa wote bila kujali masikini na tajiri.
Chonde chonde punguzeni bei kwa ajili ya masilahi ya taifa hili.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago