FIKRA ZA LEO: NEMBO YA TRAFIKI WA TANZANIA NI RUSWA

Pichani ni Askari wa Usalama barabarani ambao wameanzakuitwa Askari wala rushwa barabarani, katika jiji la Dar,ambako nako nikinara cha kula rushwa.. Picha na Maktaba.
Jana nilikuwa katika anga za kisiasa za Tanzania ila leo na wazungumzia hawa wala ruswa walio kidhiri katika hili Taifa,Kwanza kabisa kabla ama awali ya yote nakushukuru ewe Mola Muumba mbingu nchi ,sayari na dunia kwa uzima na afya tele.

Msoamaji wa safu hii ya Fikra za Leo natumai ni mzimatele,Leo asubuhi wakati nikiwa kwenye gari anaelekea kazini nilimsikia abiria mmoja akilaumu yakwamba matrafiki wamekidhiri kwa Rushwa hususani hapa Jijini Arusha na kusema ya kwamba hii yote ni shauri ya Mapaparazi yaani wanahabari kusahau wajibu wao.

Sipingani na wazo hilo ila nieleze tuu ukweli ya kwamba Nembo kubwa ya Matrafiki wa Tanzania ni KULA RUSWA.Ukitaka kumjua askari wa usalama barabarani ambao hivi sasa wanaitwa askari wala ruswa barabarini ni pale tuu atakapo kupiga mgono na kukutajia makosa huku akihitaji ruswa.
Nami baada ya kishuka kwenye gari wakati naelekea ofsini nika ona gari moja  inayofanya safari zake kwa Morombo.ikiwa imekamatwa na Trafiki wawili huku mmoja akiwa ndani na mwingine akiisindikiza kwa pikipiki.

Mara baada ya mwendo kwenye njia panda ya Stendi ya mabasi ya mikoani hapa karibu na Uwanja wa mpira wa Karume,asikari yule alishuka na kupakia kwenye pikipiki yake,juma lililopita nilikuwa safarini natoka Rombo Kilimanjaro nakuja Arusha nikiwa kwenye Noah nikamsikia dereva akilalamikia Askari hao wa maeneo ya njia panda Himo ya kwamba wamekidhiri kwa rushwa na kila Noah inayopita lazima aipige mkono,namnukuu.

"Embu fikiri Noah hapa zipo zaidi ya mia,akipiga mkono Noah mia siana zaidi ya laki ?kuna watu wanadharau hizo elufu moja nakuziona ni ndogo,lakini kwa siku akosi kama laki"
Kwa hiyo tatizo hili sio la Arusha tuu bali ni la taifa zima kwa ujumla ingawaje lipo hadi magogoni kwani kwenye Escrow wafanyakazi  wao wapo ila huku Barabarani kumezidi.

Mimi na wewe Fikra za leo zinatutaka tuchukuwe hatua tena kwa haraka na kosa ama hatia ipo kwa wote mtoaji na mpokeaji,kataa ruswa barabani kwa nzia sasa,ni bora kulipa faini ambayo itakujengea msingi wakutokukamatwa hata kama makosa ya uongo kuliko kuendekeza wizi utakao kuzuia kusonga mbele na kukufanya utoe pesa nyingi kwani kama unasafiri mwende mrefu kwa kosa hilo moja unaweza kukamatwa mara nyingi na kutoa fedha nyingi zaidi wakati ungeweza kuandikiwa na kujikuta unalipa fedha kidogo.

Nakutakia ufwatiliaji mwema wa safu hii na endelea kupata habari mbalimbali kwenye blogi hii ya HAKI LEO www.hakileo.blogspot.com
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company