Namshukuru MUNGU kwa uzima tele na kutuwezesha kukutana tena leo katika safuu hii ya Fikra za Leo na baada ya kwenda kule Burundi na jana kuwa DRC leo tunareje katika anga za sisasa za nyumbani Tanzania.
Ninayo mengi ila naomba nisema hili moja yakwamba 2015 sii lazima wawe wale wale katika uchaguzi.
Mwaka huu tuna uchaguzi mkuu utakaohusisha nyanja zote kubwa yaani Uraisi,Ubunge na Udiwani,lakini kumekuwa na kasumba katika vyama vyetu vyakupitiasha ama kutazama wagombea walewale na kuacha chipukizi wenye uwezo.
Katika vyama vyote hili lipo ila kwa Uraisi vyama vya upinzani vinaudhaifi huu zaidi,leo nimemsikia kiongozi mmoja mwenye dhamana ya habari kwenye chama cha upinzani akijaribu kujiosha ya kwamba hakuna mtu aliyeandaliwa kwa ajili ya kugombe nafasi kwenye chama.
Sitaki kupingana na fikra hizo ingawaje mwenye macho ambiwi tazama bali huambiwa ona,ila ukweli ni kwamba CHADEMA asiposimama Mbowe basi ni Dk. Slaa, ila kwa NCCR wamekwepa lawama na sasa Mbatia kakimbilia Ubunge na CUF nako Pro.Lipumba hana mpinzani.
Ukweli ni kwamba hili linadhoofisha Demokrasia ukizingatia ya kwamba siasa ni kama upepo mwaka huu huweza kuwa kule na mwaka ujao huku,sio kweli kwamba watu hawa kama Pro. Lipuma amegombania mara nyingi sio kwamba anauwezo ama mvuto usio chuja, sio kweli hata kidogo bali ni ufinyu wakimawazo na kimkakati ndio unaotusumbua.
Katika hili tujifunze kwa walio fanikiwa kwani sijawahi kuna vyama vya nchi kama Marekani vikimpitisha mgombea huyo huyo kwa chaguzi zaidi ya 4 ,lakini kwetu ni utamaduni,tuache ushamba na ulumbukeni wakisiasa.
Nihayo tuu machache tukutune tene kesho kwenye safu hii,, kwa maoni 0759859287
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago