FIKRA ZA LEO,TUACHE UNAFIKI KIKWETE UMEVUNJA SHERIA UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA WAPYA HASA KWA MAKONDAMkuu wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Paul Makonda akisaini hati baada ya kuapishwa rasmi kuwa mkuu wa wilaya hiyo leo, Anaye shuhudia ni Mkuu wa mkoa wa Meck Sadick. Picha na Venance Nestory

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Paul Makonda akisaini hati baada ya kuapishwa rasmi kuwa mkuu wa wilaya hiyo, Anaye shuhudia ni Mkuu wa mkoa wa Meck Sadick. Picha na Venance Nestory
Tuache longo-longa ama chenga nyingi ukweli ni kwamba Rais Kikwete umekiuka adharani sheria ya Utumishi wa umma inayokataza makada ama wanachama wa vyama vya siasa kufanya shuhuli za Umma sio kwa wakuu wa wilaya tuu bali hata mikoa,makatibu wa kata na vijiji na pia wanajeshi na watu wote wa usalama bila kusahau walimu na wengineo.
Lakini adharani bila hata kuwa na mshipa wa aibu Kikwete na waziri wako mkuu Pinda umeteuwa wakuu wa wilaya wapya juma lililopita na wapo ambao ni wanachama wa chama chako cha CCM miongoni mwao ni huyu Mkuu  wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.


Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la Mwaanchi la Terehe 23 mwezi huu limeandika "Mkuu huyo wa wilaya ambaye ni Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa UVCCM aliapishwa jana katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo. Baada ya kuapishwa aliingia katika kikao hicho akielezwa kuwa ameshakuwa mjumbe rasmi."
"Makonda ni kati ya wakuu wa wilaya wapya 27 walioteuliwa na Rais Kikwete takribani wiki moja iliyopita. Mbali na uteuzi huo, rais Kikwete aliteungua uteuzi wa wakuu wa wilaya 12 na kuwabadilisha vituo vya kazi wengine 64 " Mwisho wa kunukuu.
Kama huyu ni kiongozi wa chama na anateuliwa kuwa kiongozi ama mtumishi wa umma hapa haki kwa wakina CHADEMA na CUF iko wapi,hali hii ni ya hatari sana na ukizingatia kuwa hawa ndio wahusika kwenye kamati ya usalama ya mkoa na kiongozi katika kamati yake ya usalama ya wilaya,usishangae maandano ama mikutano ya vyama vya upinzani ikaendelea kukandamizwa na kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi hawa ndio wasimamizi pia katika chaguzi.
Sasa kiongozi wa CCM anasimamiaje uchaguzi ama anaongozaje hiyo timu ya uchaguzi nikiwa na maana ya tume kwenye wilaya angali yeye ni kada ama mwanachama wa chama kingine,tuache uongo na kujidanganya huu sio wakati wakufunika kombe uharamu wa CCM upite kwani kuna madhara makubwa katika kufanya hivyo.
Mimi sii nabii ila kwa mtindo huu Kikwete na Pinda musipokuwa makini mtalipeteka taifa korongoni amabako kulitoa itachukuwa miongo.Mwenye masikio na asikie,
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company