Msemaji wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) ametangaza kuwa machafuko na mapigano katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yamesababisha watu zaidi ya elfu thelathini kuwa wakimbizi. Msemaji wa UNHCR ameeleza kuwa kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za Umoja wa Mataifa, machafuko, vitendo vya ubakaji, mauaji na uporaji huko Jamhuri ya Afrika ya Kati vimepelekea watu zaidi ya elfu 30 wakazi wa nchi hiyo kuwa wakimbizi, tangu kuanza mwaka huu wa 2015 hadi hivi sasa. Watu zaidi ya elfu ishirini kati ya elfu thelathini wamekimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Msemaji wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa, raia wa kawaida ndio walengwa wakuu wa hujuma zote hizo zilizotajwa na kwamba waasi wamekuwa wakichoma moto nyumba za raia na kuwabaka wanawake na mabinti.
CHANZO IRIB SWAHILI
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago