Vikosi vya usalama vya Yemen vikiwa mbele ya ubalozi wa Ufaransa katika mji wa Sanaa, ambao ulifunga milango yake Februari 13 mwaka 2015. AFP PHOTO / MOHAMMED HUWAIS |
Idara zote za wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa zimehamasishwa ili kuhakikisha kuwa zimempta raia wa Ufaransa, aliyetekwa nya mapema Jumanne asubuhi Februari 24 nchini Yemen.
Raia huyo wa Ufaransa ametekwa nyara na watu wenye silaha katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa, wakati alipokua akisafiri kwa gari ndogo la uchukuzi (taxi).
Isabelle Prime, mwenye umri wa miak 30 ni mzaliwa wa Angers, alitekwa akiwa na raia mwengine wa Yemen. Raia huyo alikua akifanya kazi katika shirika moja la kimataifa.
Wakati huo huo rais wa Ufaransa, François Hollande, ameomba raia huyo achiliwe huru haraka iwezekanavyo.
Mji mkuu wa Yemen, uko chini ya udhibiti wa wanamgambo wa Kishia kutoka jamii ya Houthi tangu mwezi Septemba mwaka uliyopita.
Mvutano umeendelea kujitokeza kati ya watu kutoka jamii za Wasuni na Mashia, na kwa sasa nchi hiyo inakabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Balozi nyingi za nchi za magharibi zimefungwa nchini Yemen. Marekani ni nchi ya kwanza, ambayo ilianza kufunga ubalozi wake, ikieleza kuwa ni kutokana na kudorora kwa hali ya usalama katika mji wa Sanaa.