Nchini Syria zaidi ya Wakristo 80 wametekwa nyara kaskazini mashariki mwa nchi. Inasadikiwa kuwa watu hao wametekwa nyara na wanamgambo wa makundi ya kiislamu, baada ya kuvamia vijiji kadhaa katika mkoa wa Hassaké, mkoa unaopiganiwa na wanajihadi, ambao uko mikononi mwa wapiganaji wa Kikurdi kutoka Iraq.
Wengi mwa wakazi wa vijiji hivyo wameyahama makazi yao, lakini makumi ya raia hao, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, wanasadikiwa kutekwa nyara na wanajihadi.
Kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu nchini Syria (OSDH) pamoja na mashirika mengi ya Kikisto yanayoendesha harakazi zao Ulaya na Amerika ya Kaskazini, wanamgambo wa kundi la wapiganaji wa Dola la kiislamu (IS) wamevamia vijiji kadhaa vinavyopatikana kusini mwa mto Khabour, eneo linalopatikana katika uwanja wa mapigano, ambalo linagawa wapiganaji wa Kikurdi kutoka Syria na mahasimu wao wa IS.
Shambulio hilo lilinaaminika kuwa limeendeshwa mapema Jumanne asubuhi wiki hii. Familia kadhaa zilikimbia eneo hilo mapema, kwa kuhofia kuuawa na wanamgambo hao. Hata hivyo wapiganaji wa IS wamewateka nyara watu walio kati ya 90 na 200, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali.
Kwa mujibu wa shirika la misaada kwa raia wa Syria ADFA, wanaume wametenganishwa na wanawake pamoja na watoto.
Inaaminiwa kuwa wapiganaji wa IS wameomba kubadilishana wafungwa na wapiganaji wa Kikurdi wanaoshirikiana na wanamgambo wa Kikristo.
Kwa mujibu wa taarifa ambayo tuliyonayo, mapigano makali yanaendelea katika eneo hilo. Mapigano ambayo yalisababisha raia kuyahama makazi yao na kukimbilia kaskazini na katika maeneo ya Wakurdi kutoka Syria, ambayo yako mbali na wapiganaji wa Dola la Kislamu.CHANZO:I.R.F
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago