Waziri wa Uchukuzi ,Samweli Sita akitangaza kumfuta kazi aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini,Madeni Kipande kutokana ubadilifu katika utoaji wa dhabuni Dar es Salaam jana.Picha Na Said Khamis
Na Nuzulack Dausen, Mwananchi
KWA UFUPI
Hatua hiyo ya Sitta imekuja wiki tatu baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuiongoza wizara hiyo akitokea Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla, wizara hiyo ilikuwa chini ya Dk Harrison Mwakyembe.
Dar es Salaam. Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande baada ya kuwepo malalamiko ya ubabaishaji katika zabuni mbalimbali za mamlaka hiyo.
Hatua hiyo ya Sitta imekuja wiki tatu baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuiongoza wizara hiyo akitokea Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla, wizara hiyo ilikuwa chini ya Dk Harrison Mwakyembe.
Sitta, ambaye pia hujulikana kama Mzee wa Viwango, amewaambia waandishi wa habari jijini hapa leo kuwa wadau mbalimbali wamesema taratibu za zabuni TPA haziendeshwi kwa uwazi na uaminifu.
“Wanasema hakuna uwazi katika zabuni, kuna dalili ya ubabaishaji. Katika kamati za kutathmini zabuni majina ya watu yanabadilika badilika na hata baada ya mshindi kupatikana bodi huchelewa kutoa barua inayohusu uamuzi wa kumpata mshindi huyo,” amesema Sitta.
“Hayo yote yanajenga taswira isiyo nzuri kwa bandari, serikali na nchi nzima kwa ujumla,”
Kwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji ndiye msimamizi mkuu wa shughuli za bandari, amesema ameamua kumsimamisha Kipande kupisha uchunguzi kwa kipindi hicho na nafasi yake itachukuliwa na Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Awadh Massawe.
Kutokana na kusimamishwa kwa kigogo huyo, Sitta aliitangaza tume maalumu ya watu sita itakayochunguza tuhuma hizo ikiongozwa na Jaji Mstaafu Augusta Bubeshi na itafanya kazi hiyo kwa majuma mawili.
Wengine katika tume hiyo ni Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA) Dk Ramadhan Mlinga, Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa TPA Samson Luhigo, aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu, TPA Happiness Senkoro.
Pia, katika tume wapo Mkurugenzi wa Masoko mstaafu wa TPA Flavian Kinunda na Mtumishi wa Wizara ya uchukuzi Deogratius Kassinda atakaye kuwa Katibu.
“Nimejitahidi kuwachukua hawa wastaafu kwa kuwa kwa sasa hawatafuti cheo chochote na tunaamini watatenda haki kwa kuchunguza tu bila uonevu wowote.
“Ni muhimu sana taratibu za bandari ziwe wazi, ziheshimike duniani kote kwa kuwa miradi ya bandari ni mikubwa sana inayopitishwa na bodi ya zabuni ya bandari,” amesema Sitta
Hata hivyo Waziri Sitta baada ya kumaliza kuzungumza na waandishi hakutaka kuruhusiwa kwa swali lolote kwa madai kuwa anamajukumu mengine.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago