Jerry Muro. |
Alichokijibu kwanza kuhusu familia; “Nna mke.. watoto hapana, ni suala la muda na wakati kujipanga. Hawa ambao wana watoto sasa hivi hawakukosea lakini hata ukiangalia mfumuko wa watoto wengi Panya Road wametoka wapi. Mtoto akipatikana kwa wakati sahihi na ukimleta duniani kwa malengo sahihi hawezi kwenda kuwa Panya Road“
Salama Jabir na Muba
Kuhusu ishu ya watu kukimbia taaluma ya ualimu; “zamani wakati tunakua tukienda Kijijini tunaambiwa ‘ile ni nyumba ya mwalimu’, zamani mtu kuwa mwalimu alikuwa na nafasi kubwa kwenye jamii kuliko hata Waziri.. Ualimu wa Nyerere ndio ulimpa nafasi kubwa sana tangu ameanza harakati zake mpaka kushika madaraka.. Hakuna jambo tulilikosea na hatutasamehewa kwa Mungu tulipoamua kubinafsisha sekta nyeti sana, elimu na afya“
Suala la kugombea Ubunge; ” Naamini kiongozi bora ni yule ambaye amesha demonstrate tangu mwanzo kabisa na ameshaonyesha vitu ambavyo vinaashiria huyu ni kiongozi. Mimi sijisemi kuw ni kiongozi mzuri kwa wale wanaojua kazi nilizozifanya kipindi kile niko kwenye uandishi wa habari nili demonstrate“
Salama Jabir
Kuhusu ishu ya kesi ya Rushwa; ” Mimi sikuomba rushwa nikakamatwa.. askari mmoja akahoji hapa tunaandikaje, tunakupa dhamana kwa kosa gani?
Baadaye nikaenda Mahakamani ikasomewa niliomba Rushwa.. Kwenye kesi yangu wakati Hakimu anatoa ruling alisema hapakuwa na ushahidi wa mimi kuomba rushwa..“
Sijawahi kuomba Rushwa lakini nimekutana na mazingira mengi ya kupewa Rushwa. Mimi ni mwandishi wa kwanza wa pekee wa television kuonesha mtu mwenye dhamana ya Serikali.. mwenye crown akila rushwa hadharani.. Nilifanya hiyo nikiwa ITV, baadhi ya watu wakasema huyu si ameotea tu.. Nilipoenda TBC nikafanya tena story ileile nikarusha.. Tangu nilipomaliza kesi yangu mpaka leo sijaajiliwa na mtu yoyote“
.
Hapa alizungumzia mapenzi yake na Klabu ya Yanga yalikoanzia; “Mapenzi na Yanga yalianzia kwa baba yangu.. Baba yangu alikuwa anapenda Yanga.. Ukifanya utafiti wa juu juu tu katika nchi zilizo kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki Tanzania inaongoza kuwa na mazingira mazuri sana ya mchezo wa mpira wa miguu. “
Nimekurahisishia kwa kukuwekea hii sauti hapa, bonyeza play kuisikiliza sehemu ya Interview hiyo..