Zitto ataka kampuni ya umma bandari ya Dar

Mkuu wa Kitengo cha Mafuta Bandari ya Dar es Salaam, Nahodha Abdallh Mwingamo (Kulia) akielezea namna ya upakuiaji wa Mafuta wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipotembelea Bandarini jana. Picha na Said Khamis
Na Laura Paul, Mwananchi Online
KWA UFUPI
Kama hiyo haitoshi Kabwe amekwenda mbali Zaidi kwa kuutaka uongozi wa bandari kupunguza maneno na mipango isiyotekelezeka badala yake wafanye kazi kwa bidii ili kupunguza kero lukuki zinazoiandama mamlaka hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Zitto Kabwe amependekeza kuanzishwa kwa Kampuni ya umma itakayokuwa inahusika kufanya shughuli za kupakia na kupakua mizigo katika bandari ya Dar es Salaam badala ya utaratibu wa sasa ambao ni wa kampuni binafsi.

Kama hiyo haitoshi Kabwe amekwenda mbali Zaidi kwa kuutaka uongozi wa bandari kupunguza maneno na mipango isiyotekelezeka badala yake wafanye kazi kwa bidii ili kupunguza kero lukuki zinazoiandama mamlaka hiyo.

Kabwe ameyasema hayo leo baada ya yeye na kamati nzima ya PAC kutembele bandari hiyo kwa lengo la kutaka kujua namna ya utozwaji wa kodi , maendeleo ya ujenzi wa mabomba ya kusambazia mafuta na mradi wa uboreshwaji wa maboya unaoendelea bandarini hapo.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo baada ya kujionea shughuli zima zinavyofanywa Mwenyekiti Kabwe amesema ifike mahali bandari ya Dar es Salaam ikawa na kampuni ya Umma inayofanya shughuli zote za kibandari, akitolea mfano wa nchi ya Kenya kwamba wanayo Kampuni ya Umma kwa upande wa bandari ambayo inaitwa KBC.

Kabwe amesema upo uozo katika bandari hiyo ambao kama usipotatuliwa bandari hiyo itakuwa ikipata hasara kila mwaka hivyo ni lazima watendari wa Serikali wanaofanya vibaya waweze kuwajibishwa ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi kwa manufaa ya umma.


Naye Meneja wa TPA Awadhi Masawe amesema tatizo la kutokuwa na kipimo kinachoonyesha idadi ya mafuta kabla ya kupakuliwa, linasababisha usumbufu mkuwa, hivyo aliomba na kuitaarifu kamati hiyo kuwa umefika wakati kuwe na kipimo cha mafuta.

“Tunatamani meli ya mafuta ikiwa imekuja watendaji waweze kutambua ni kiasi gani cha mafuta yaliyo letwa na meli hiyo, hii italeta ufanisi Zaidi katika utendaji wa siku kwa siku’,” amesema Massawe.

Pamoja na hayo Kabwe alisisitiza na kuwataka wafanyakazi wa bandari hiyo kuchapa kazi na kufanya biashara ya mafuta na nchi zote za karibu, akiwaeleza kuwa ujenzi wa geti namba 13 na 14 lazima ukamilike haraka kwani hivi sasa bandari ya msumbiji wameshakamilisha ujenzi wa geti hizo
CHANZO MWANCHI
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company