JOSEPH KABILA |
Unajua wanasema mtu mzima akosei labla huwa anapitiwa ila hii ni lugha ya kinafiki wala haina kweli ndani yake,,na mimi sio mnafiki kwahiyo nasema Kabila kwa hili umekosea,,ama kama huja kosea basi kunanjama ya siri iliopo hapa.
Unajua wanasiasa wengi ni wanafiki na kwao kutawala kunadhamani kuliko maisha ya watu na yamkini ndio maana kikundi hiki kingali bado kipo hadi leo.SASA KAMA JESHI LAKE LINAWEZA KUKIPIGA MBONA MIAKA YOTE HIYO ASIKIPIGE.
Fikra za leo zinatamka bayana ya kwamba huyu ana mchezo anataka aufanye ukuzingatia ya kwamba mwaka huu kuna uchaguzi na ukombioni kufanyika yamkini anataka akitumie kama sababu ya kuvuruga uchaguzi huo ili aendelee kupeta madarakani.
Ila ni mwambie tuu yakwamba uchaguzi wa mwaka huu wala haumuhusu maana muda wake umekwisha na kamwe asijidanganye ya kwamba jeshi lake lina ubavu wakupigana na kikundi hiki maana kwa miaka mingi ameshindwa kufanya hivyo na tumesha jua ya kwamba anataka akitumie kama mtaji wake wakisisa.
Nazitaka zile nchi na umoja wamataifa zilizojiandaa kupambana na waasi hawa wasikate tamaa na wagunduwe tuu hayo ni maneno ya mtu alipoteza mwelekeo wa kisiasa,,pia ni mwambie amalizane na M23 maana kiongozi wake bado yupo Uganda na wenzake amasivyo asije akalia kilio kilichokosa wazazi maana maadui zake kisiasa yaani RWANDA na Raisi wa UGANDA wangali wanaishi na Rafiki yake kisiasa TANZANIA amejaa unafiki kwahiyo atamkwepa.