WAZIRI LUKUVI APOKEA MWENYEWE KERO ZA ARDHI RUKWA!

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, akipokea na kuchambua barua za malalamiko ya wananchi kuhusu migogoro ya ardhi mkoani Rukwa leo hii. Zoezi hilo ameliendesha mwenyewe katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na kuwaagiza maofisa wake kuyashughulikia malalamiko hayo huku akiwaahidi wananchi hao kwamba yatapatiwa ufumbuzi baada ya mwezi mmoja. (Picha zote na brotherdanny5.blogspot.com).



Msururu wa wananchi wakiwasilisha barua na vielelezo vya malalamiko yao kwa Waziri Lukuvi leo hii mjini Sumbawanga.

Waziri Lukuvi akikagua malalamiko hayo kuona kama yanastahili kushughulikiwa na wizara yake ama la.

Waziri Lukuvi akirejesha vielelezo kwa mwananchi mmoja na kuelekeza kwamba kwa vile suala hilo lilikwishapita mahakamani, basi aende katika mahakama za juu kwani Serikali haiwezi kuingilia uamuzi wa mahakama.




Hata mfanyabiashara maarufu wa mjini Sumbawanga, Aziz Tawaqal naye aliwasilisha malalamiko yake ya kudhulumiwa ardhi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company