Jeshi Sudan Kusini ladhibiti mji wa kistratijia wa Leer

Serikali ya Sudan Kusini, imetangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kudhibiti mji muhimu wa Leer uliokuwa ukidhibitiwa na waasi. Taarifa iliyotolewa jana na serikali hiyo imesema kuwa, udhibiti wa mji huo umejiri kufuatia operesheni kali za jeshi hilo, zilizoambatana na wapiganaji wa waasi kukimbia mjini humo. Serikali ya Sudan Kusini imeongeza kuwa, operesheni za kuusafisha mji huo kutokana na uepo wa waasi, zimejiri ikiwa ni katika stratijia za kuidhibiti miji iliyopo katika jimbo la Unity kaskazini mwa nchi hiyo changa zaidi barani Afrika. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mapigano makali yamejiri baina ya vikosi vya serikali na waasi katika viunga vya mji wa Malakal kaskazini mashariki mwa Sudan Kusini. Mapigano nchini Sudan Kusini yaliibuka mwezi Disemba mwaka 2013, baada ya rais wa nchi hiyo Salva Kiir kumtuhumu aliyekuwa makamu wake, Riek Machar kwa kutaka kumpindua madarakani. Hadi sasa makumi ya maelfu ya watu wamekwishauawa huku zaidi ya watu milioni mbili wakiwa wakimbizi. Sudan Kusini ilijitenga na Sudan hapo mwaka 2011 na kujitangazia uhuru wake. Licha ya jamii ya kimataifa kuingilia kati mgogoro huo na kutishia kuwawekea vikwazo vinara wa pande hasimu, lakini juhudi hizo hazijazaa matunda katika kuhitimisha hali ya mchafukoge nchini humo.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company