Lavrov: Saudia ikomeshe jinai zake Yemen mara moja

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov ametaka kukomeshwa kikamilifu mashambulizi ya Saudia na waitifaki wake nchini Yemen haraka iwezekanavyo. Lavrov ameyasema hayo alipokutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Oman, Badr bin Hamad Bu Said, na kusisitiza kuwa, Moscow inataka kuhitimishwa umwagaji damu huo mkubwa nchini Yemen na kwamba kutiwa saini makubaliano ya usitishaji vita ni suala la dharura. Aidha amesisitizia umuhimu wa kuanza mchakato wa utatuzi wa kadhia ya Yemen kisiasa, kupitia mazungumzo ya kitaifa chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa. Katika kikao hicho baina ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Oman, viongozi hao wamejadili kwa upana hali ya eneo la Ghuba ya Uajemi yakiwemo masuala muhimu baina ya pande mbili hizo sanjari na kusisitizia udharura wa kuimarishwa ushirikiano wa kisiasa kati ya Muscat na Moscow. Mashambulizi ya Saudia na waitifaki wake zikiwemo, Marekani, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, Ufaransa na nchi nyingine za Kiarabu dhidi ya Yemen, yalianza tangu tarehe 26 mwezi Machi mwaka huu, ambapo mbali na kushindwa kufikia malengo yake, yamepelekea maelfu ya watu kuuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa na kuharibiwa miundombinu mbalimbali nchini humo.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company