RAIS Jakaya Kikwete amesema Serikali inafanya mazungumzo na Ofisi ya Spika wa Bunge kuongeza siku 10 za kuwasilisha miswada mbalimbali.
Kauli hiyo aliitoa juzi mkoani Arusha alipofungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ambao ulikuwa pamoja na uchaguzi wa nafasi za juu za chama hicho.
Akizungumza katika mkutano huo ulikuwa na wajumbe zaidi ya 1,200 ambako mke wake Salma Kikwete pia alihudhuria, Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuwaaga walimu hao.
Katika hotuba yake iliyojibu zaidi maombi ya walimu, Rais Kikwete aliwaambia Serikali inaendelea na mazungumzo ya kuongeza siku ili kuwasilisha bungeni Muswada wa kuanzisha Bodi ya Taifa ya Taaluma za Walimu (National Teachers Professional Board).
“Tunaendelea na mazungumzo na Ofisi ya Spika tuweze kuongeza siku 10 bungeni zitakazokuwa kwa ajili ya miswada,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Siku hizi tumepanga na Spika kwamba Serikali ndiyo itakayozigharamia. Na tutakubaliana kabisa muswada wa kwanza uwe wa kuanzishwa Bodi ya Taifa ya Taaluma za Walimu,” alisema.
Huku wakimuita shemeji, shemeji, Rais Kikwete aliwaeleza kuwa Serikali ilikwisha kupeleka bungeni Muswada wa Sheria ya kuanzisha Tume ya Utumishi wa Walimu (Teachers Service Commission) na ulikwisha kusomwa kwa mara ya kwanza.
“Ninawapenda, nimewapenda na nitaendelea kuwapenda Shemeji zangu. Kwa sababu natambua mambo yaliyowasilishwa ni ya msingi yanahitaji kufanyiwa kazi,” alisema Rais Kikwete
Awali akisoma risala ya walimu hao, Katibu Mkuu wa CWT Alhaj Yahaya Msulwa, alimuomba Rais Kikwete kabla ya kuondoka asaini kuwa sheria, Muswada wa kuanzisha Tume ya Utumishi wa Walimu (Teachers Service Commission).
Alhaji Msulwa alimueleza Rais Kikwete matatizo sugu yanayowakili walimu nchini kwa miaka mingi ambayo ni uhaba wa walimu hasa wa sayansi, madeni ya walimu na posho ya kufundishia.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago