MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) jana nusura apigane na askari aliyekuwa akilinda kituo cha kujiandikisha katika daftari la wapiga kura cha Shule ya Msingi Mkombozi Kata ya Sokoni I.
Tafrani hiyo ilitokea saa 5.00 asubuhi wakati Mbunge huyo
alipokuwa akitembelea vituo vya kujiandikisha kupiga kura jijini Arusha akifuatana na waandishi wa habari. Uandikishaji huo ulianza juzi.
Lema alipofika kituoni hapo alikuta foleni kubwa nje ya lango la kuingia kituoni hapo huku ndani ya lango hilo akiwamo askari wa kike aliyekuwa amevalia kiraia.
Askari huo alikuwa akiandikisha majina ya wananchi hao na kuwataka waondoke hadi kesho yake kupata vitambulisho.
Kutokana na hali hiyo Lema alibishana na askari huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana na kumnyang’anya kalamu aliyokuwa akitumia kuandika majina hayo katika daftari dogo huku akiwaambia polisi hao wanavunja sheria.
Majibizano kati ya Lema na askari huyo wa kike yalisababisha askari mwingine wa kiume kuingilia kati na baada ya mabishano makali na Lema, walishikana wakitaka kupigana kabla ya kuamriwa na viongozi waliokuwa wamefuatana na Lema.
“Haiwezekani polisi akaandikisha majina na kuwaambia watu waje siku inayofuata waweze kufanya taratibu za kupewa vitambulisho.
”Polisi wajibu wako hapa kituoni ni kuangalia usalama na siyo vinginevyo, utaratibu mnaoufanya ni kosa. Hata mawakala wa vyama vya siasa waliopo hapa hawana majina haya.
“Tutajuaje mnaenda kuyabadilisha au kuuza hili daftari na kutuletea majina mengine ... na daftari hili halina muhuri wa aina yoyote,”alisema Lema.
Tafrani hiyo ilisababisha Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha (OCS),Thomas Mareko kufika kituoni hapo naye akaendelea kubishana na Lema aliyesisitza kuwa polisi walikuwa wanafanya makosa.
Hatimaye mmoja wa wawakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha alifika kituoni hapo na kuzungumza na Mbunge huyo pamoja na OCS pembeni.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago