Muhammed Morsi, rais wa zamani wa Misri aliyehukumiwa kifo kwa makosa kula njama ya kutorosha wafungwa katika vuguvugu la mageuzi katika nchi za Kiarabu mwaka 2011 |
Jaji Shaaban al-Shamy alisoma hukumu dhidi ya Bwana Morsi na watuhumiwa wenzake kadha kutoka kundi la Muslim Brotherhood. "Mahakama kwa kauli moja imeamua, kwanza kwa wale waliofika mahakamani, kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa washitakiwa Muhammad Badi Abd-al-Majid Sami, Rashad Muhammad Ali al-Bayumi, Muhyi Hamid Muhammad al-Sayyid Ahmad, Muhammad Sa'd Tawfiq Mustafa al-Katatni, Muhammad Muhammad Morsi Isa al-Ayyat, Isam-al-Din Muhammad Husayn al-Iryan."
Hata hivyo Marekani imesema imesikitishwa sana na hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama ya Misri dhidi ya rais wa zamani Mohammed Morsi.
Ikulu ya Marekani imeielezea hukumu hiyo kuwa na msukumo wa kisiasa. Naye Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon pia ameelezea kusikitishwa na hukumu hiyo.