Rais Vladimir Putin (kushoto) akiongozana na jenerali Sergei Shoigu wakati wa kuwasili kwake katika makao makuu ya jeshi "Jeshi-mwaka 2015". Kubinka, Juni 16 mwaka 2015.
Na RFI
Wakati ambapo Pentagon ilipendekeza Jumatatu wiki hii kuweka silaha nzito katika baadhi ya nchi za Ulaya Mashariki, siku ya Jumanne, rais wa Urusi Vladimir Putin ametumia fursa ya mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Armia 2015 kwa kuweka hadharani baadhi ya zana za kisasa za vikosi vya jeshi la Urusi.
Putin ametangaza kuwa Urusi itaimarisha zana zake za nyuklia.
Rais wa Urusi, Vladmir Putni, ametangaza kuwa Urusi itaongeza zaidi ya makombora 40 ya kinukilia yanayoweza kufikia mabara mbalimbali duniani kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Alisema kuwa makombora hayo mapya yatakuwa ya kisasa yatakayoweza kukwepa vifaa maalumu vya kukabiliana na aina zozote za silaha.
Serikali ya Urusi inaonekana kutokubaliana na mpango wa Marekani ambayo imeanza kubadilisha maeneo yaliyoegezwa vifaru vyake na magari mengine ya kivita katika maeneo yaliyo karibu na Urusi.
Hatua hii inaonyesha wazi kuwa Urusi imechukulia vibaya sana mazoezi ya kijeshi ambayo yameimarishwa na mataifa wanachama wa muungano wa kujihami wa NATO katika mataifa ya Poland na Baltic.
Hatua ya kuanzisha mazoezi ya kijeshi katika maeneo hayo ilichukuliwa na Marekani, kufuatia hatua ya Urusi ya kujinyakulia eneo la Crimea na kuiingiza majeshi yake katika maeneo mengine ya Ukraine.
Katika juhudi za kuonyesha ubabe wake dhidi ya mataifa ya Magharibi kufuatia kuimarika kwa uhasama kati yao, Rais Putin ameamua kuimarisha zana zake za kinukilia.
Hatua hii inaonyesha dhahiri kuwa zana za kisasa za kivita zimeanza kupungua nchini Urusi.
Urusi tayari imeanza kubadili silaha zake zote ili zifikie viwango vya kisasa.
Hata hivyo rais wa Urusi pia ametangaza kuanzishwa kwa mfumo wa rada, ambayo inaweza kuchunguza maadui zake katika umbali mrefu sana, ambayo itakuwa ikigeuzwa kuelekea nchi za Magharibi. Vikosi vya jeshi la Urusi pia vitakuwa na vifaa na mizinga, ambavyo " havipatikani duniani " amesema Vladimir Putin.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago